Jumanne 2 Desemba 2025 - 07:00
Israel Yatumia vyombo vya Habari Kama Nyenzo Dhidi ya Waislamu Ufaransa

Hawza/ Hivi karibuni kura ya maoni ilichapishwa nchini Ufaransa ambayo iliandaliwa kwa kuungwa mkono na Mayahudi na hatimaye Israel dhidi ya Waislamu wa Ufaransa, lakini nyaraka zilizopatikana zinaonesha juhudi za Israel za kuleta mtikisiko katika jamii ya Waislamu barani Ulaya.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, kutokuwepo kwa msimamo unaofaa na wa kuizuia Israel dhidi ya uhalifu wake wa kinyama huko Ghaza kumesababisha utawala huu wa haramj kuvuka mipaka zaidi na kuchukua hatua dhidi ya Waislamu wa maeneo mengine ya dunia pia; hali ambayo matokeo yake mabaya yatazikumba tabaka zote za jamii.

Wakati ambapo maoni ya umma nchini Ufaransa bado yanayumbishwa na kashfa ya kura ya maoni dhidi ya jamii ya Waislamu iliyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Maoni ya Umma ya Ufaransa (Ifop) chini ya usimamizi wa Mayahudi wenye misimamo mikali, nyaraka zimechapishwa zinazoonesha kuwa Mossad, kwa kushirikiana na Mayahudi wenye itikadi kali wanaoishi Ufaransa, ilikuwa ikifanya ujasusi na ukusanyaji wa taarifa kuhusu Waislamu pamoja na hali zao za kazi na maisha, na kisha kuziwasilisha taarifa hizo zilizokusanywa kwa Israel.

Baadhi ya makadirio yanaonesha kuwa taarifa hizo zilikusanywa kutoka katika tabaka zote za jamii. Kwa mujibu wa Baraza la Waislamu wa Ufaransa, uchunguzi huu ulisimamiwa na watu wawili, mmoja wao akiwa wakala wa maslahi ya Wazayuni. Kura hiyo ya maoni, katika taarifa iliyotolewa na baraza hilo, ilielezewa kuwa ni “hatari na isiyo na mfano,” na ikasisitiza kuwa; taarifa hizo zimefichuliwa katika wakati nyeti sana. Imeelezwa kuwa vitendo hivi vinaandaliwa mfululizo na Wazayuni, na vyombo vya habari vinasukumwa kuelekea uenezi wa matangazo ya kibaguzi na ya kirasimu dhidi ya Waislamu na Uislamu.

Taarifa hiyo ilitolewa na Baraza la Waislamu wa Ufaransa, na ikasambazwa kwa wingi baada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mtu aliyedai kuitwa Didier Lang alifichua kwamba tangia mwanzoni mwa mwaka 2023 alikuwa akifanya utafiti na kazi juu ya jamii ya Waislamu wa Ufaransa na njia za kuzusha mgogoro wa kimedia dhidi yao, na kwamba alikuwa amekutana na Waislamu wengi waliokuwa na nyadhifa za uwajibikaji.

Chanzo: Imenukuliwa kutoka Shirika la Habari la Al-Shorouq

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha